Jeremiah 50:3-9

3 aTaifa kutoka kaskazini litamshambulia,
na kuifanya nchi yake ukiwa.
Hakuna hata mmoja atakayeishi ndani yake,
watu na wanyama wataikimbia.

4 b“Katika siku hizo, wakati huo,”
asema Bwana,
“watu wa Israeli pamoja na watu wa Yuda
wataenda wakilia ili kumtafuta Bwana Mungu wao.
5 cWataiuliza njia iendayo Sayuni
na kuelekeza nyuso zao huko.
Watakuja na kuambatana na Bwana
katika agano la milele
ambalo halitasahaulika.

6 d“Watu wangu wamekuwa kondoo waliopotea;
wachungaji wao wamewapotosha
na kuwasababisha kuzurura
juu ya milima.
Walitangatanga juu ya mlima na kilima,
na kusahau mahali pao wenyewe pa kupumzikia.
7 eYeyote aliyewakuta aliwala;
adui zao walisema, ‘Sisi hatuna hatia,
kwa kuwa wao walitenda dhambi dhidi ya Bwana, malisho yao halisi,
Bwana, aliye tumaini la baba zao.’

8 f“Kimbieni kutoka Babeli;
ondokeni katika nchi ya Wakaldayo
tena kuweni kama mbuzi wale waongozao kundi.
9 gKwa maana nitaamsha na kuleta dhidi ya Babeli
muungano wa mataifa makubwa kutoka nchi ya kaskazini.
Watashika nafasi zao dhidi yake,
naye kutokea kaskazini atatekwa.
Mishale yao itakuwa kama mishale ya mashujaa walio hodari,
ambao hawawezi kurudi mikono mitupu.
Copyright information for SwhNEN